Rais huyo wa zamani, alikuwa akipambana na Naibu wa Rais Kamala Harris, pamoja na wagombea huru wawili Jill Stein na Robert Kennedy.
Source: Flickr / Gage Skidmore - Flickr
Naibu wa Rais Harris, alisisitiza katika hotuba yake umuhimu wa demokrasia naku heshimu matokeo ya uchaguzi pamoja naku rahisisha mchakato waku kabidhi mamlaka.Kufikia sasa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Marekani yana onesha Donald Trump alipata 50.7% ya kura, Kamala Harris 47.7% ya kura, Jill Stein 0.5% na Robert Kennedy 0.5 ya kura. Katika jimbo la Minnesota, Huldah Momanyi Hiltsley amekuwa mzawa wa kwanza wa Kenya kushinda uchaguzi na atakuwa mwanamke wa kwanza mweusi ambaye amechaguliwa kuhudumu ndani ya Seneti katika historia yake ya miaka 164.