Polisi wamtambua mshambuliaji katika mauaji ya watu wengi ambako watu sita walifariki

Westfields Bondi Junction after a critical incident with multiple casualties April 13, 2024 Photo Domenico Gentile SBS Italian.jpeg

Jeshi la polisi la New South Wales lime anza uchunguzi kwa shambulizi la kisu, lililo wauwa watu sita ndani ya soko kubwa katika vitongoji vya mashariki ya Sydney.


Polisi wamesema mshambuliaji aliyehusika katika shambulizi hilo, alikuwa ni mwanaume mwenye miaka 40, mwenye matatizo ya afya ya akili na hana uhusiano wowote na ugaidi.

Wakaaji wa Sydney wana endelea kukerwa baada ya shambulizi katika moja ya soko kubwa mjini humo mchana wa Jumamosi 13 Aprili, ambako watu sita wali uawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Mwanaume mmoja ali ingia ndani ya soko la Westfield Bondi Junction mida ya saa 9:20 mchana na, kuanza kudunga waemeaji kwa kisu, nakutengeza mazingira ya machafuko.

Jeshi la Polisi la New South Wales liliwasili katika sehemu ya tukio na hatimae afisa wa jeshi la polisi alipiga risasi naku muuwa, baada ya onyo kadhaa kwa mwanaume huyo ajisalimishe.

Waziri Mkuu amesema amepokea salamu za pole kutoka kwa viongozi wa dunia usiku wakumakia, ambao walikemea tendo hilo la vurugu.

Kasri ya Buckingham nayo ilitoa taarifa ambako Mfalme Charles III na mkewe Camilla, wali elezea huzuni yao kwa shambulizi hilo la kisu.

Naye waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, Rais wa Marekani Joe Biden na Papa, walituma salamu za ushikamano kwa familia zilizo athiriwa kwa shambulizi hilo.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Polisi wamtambua mshambuliaji katika mauaji ya watu wengi ambako watu sita walifariki | SBS Swahili